Posts

Showing posts from February, 2017

JUA NAMNA YA KUTIBU VIDONDA VYA TUMBO (ULCER)

Image
JUA NAMNA YAKUTIBU VIDONDA VYA TUMBO (ULCER) Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kupunguza uzalishaji wa asidi tumboni au mwilini kwa ujumla. Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu. Ikiwa matatizo kama kuvuja damu au vitobo sehemu ya kidonda yatatokea, basi hapo upasuaji huwa ni muhimu. Vidonda vya tumbo kwa ujumla hupona ndani ya wiki 4 mpaka 6 za matibabu. Mtu mwenye vidonda vya tumbo ni mtu mwenye asidi nyingi mwilini kuliko alkalini, hivyo anatakiwa kupendelea zaidi kula matunda na mboga za majani. Anahitaji zaidi ukijani mwilini mwake. Pia apendelee kula ugali wa dona kuliko ugali wa sembe na inashauriwa pia kupunguza kula wali. Kitu kingine mhimu kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo ni maji. Hakikisha unakunywa kila siku maji glasi 8 hadi 10. MAZOEZI MAALUMU KWA ANAYESUMBULIWA NA MIGUU KUWAKA MOTO AU ASIDI KUZIDI MWILINI Unalala chali, nyoosha mikono chini. Kis...